Milio ya risasi na milipuko Sudan Kusini

Kumemesikika milio ya risasi na milipuko katika mji wa Juba Sudan Kusini taarifa zinaeleza.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Juba wanasema baadhi ya wafanyakazi wake wameshindwa kutoka huku mashambulizi yakiwa bado yanaendelea.

Waandishi wa habari wanasema bado haijajulikana nini kinachoendelea lakini inaonekana milio hiyo ya risasi inatokea kwenye maeneo ya nyumba za jeshi.

Balozi za Uingereza na Marekani katika mji wa Juba zimewataka raia wa nchi zao kubaki ndani ya nyumba za na kuchukua tahadhari.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kwa kadri tutakavyozipata