Kuna mfano wa Mandela duniani?

Nelson Mandela daima alitajwa kama 'kiongozi mkongwe wa dunia' ambaye alikuwa na ujuzi wa kutatua matatizo ya kidunia. Sifa yake ya madili mema ilimfanya kuonekama kama mrithi wa Mahatma Gandhi. Nani sasa anaweza kuchukua majuku ya Mandela?

Maswala ya Lockerbie, Burundi, DR Congo, Lesotho, Indonesia, Israel-Palestine, Kashmir, Mauaji ya Stephen Lawrence, uhamasisho wa Ukiwmi na kombe la dunia.

Orodha ya mambo aliyoyaweka karibu naye Mandela ni ndefu.

Katika baadhi ya mizozo kama mgogoro wa muda mrefu nchini Burundi alikuwa mpatanishi.

Maswala kama Ukimwi, alikuwa mwanaharakati na baba aliyepoteza mwanawe kwa maradhi hayo.

Mchango wake ulikubalika na ukakaribishwa sana.

Alipinga kuingiliwa kati mzozo wa Kosovo mwaka 1999 na kukosoa sera ya kigeni ya Marekani, wakati huo uhusiano wake na Kanali Gadaffi na aliyekuwa Rais Suharto haukuchukuliwa kwa wema.

Wengi walihisi kuwa alichelewa katika harakati zake dhidi ya ukimwi nchini Afrika Kusini.

Lakini wakosoaji wake wanakubali kuwa alikuwa kiongozi asiyekuwa na mfano wake duniani.

Alikuwa kiongozi ambaye watu walikuwa na matumaini naye, mtu ambaye alitoa mfano wa kuigwa duniani.

Mandela alionekana kama mtu aaliyweza kukabidhiwa majukumu na kuyafanya kwa kuzingatia ukweli kwani safari yake Jakarta ambako mwanasiasa wa Timor Mashariki alikuwa amezuiliwa mwaka 1997 ilipelekea kufanyika kwa kura ya maoni na kuachiliwa kwa mfungwa huyo Gusmao miaka miwili iliyofuata.

Alikuwa na maadili ya hali ya juu sana ambayo yanaweza kuwa funzo kwa wanasiasa wote duniani wasiokuwa na mwelekeo mwema na yote yalitokana na vita vyake dhidi ya utawala wa kibaguzi miaka ya themanini.

Kumekuwa na marais wengine wakongwe lakini wao walikuwa watu ambao siasa zao zilihusu maswala ya ndani ya nchi zao.

Mfano Jimmy Carter alitumwa Korea Kaskazini kuzungumzia maswala muhimu na pia amekuwa akijihusisha na maswala ya demokrasia barani Afrika lakini hana hisia alizokuwa nazo Mandela kuhusiana na maswala kadhaa kama Mandela alivyokuwa.

Tony Blair alijaribu kujihusisha na juhudi za upatanisho Mashariki ya kati lakini wengi waliona kama alikuwa anajaribu kujifutia historia mbaya aliyo nayo kuhusu vita vya Iraq.

Lakini jambo ambalo litasalia vichwani mwa wengi ni Mandela alipoamua kutangaza kuwa mwanawe amefariki kutokana na Ukimwi mwaka 2005. Hii ilikuwa mapema wakati ambapo Ukimwi ulikuwa umekuwa donda sugu Afrika Kusini. Mandela aliwataka wananchi wa taifa hilo kuweka wazi maswala ya Ukimwi.

Unaweza kwenda popote duniani na picha yake na hakuna asiyemfahamu . Hakuna mfano wa Mandela. Aung San Suu Kyi labda kidogo anaonekana kuwa kama Mandela lakini sio rahisi kwake kutambulika kama alivyotambulika Mandela.

Gandhi, Mandela na Suu Kyi walikuwa wafungwa wa kisiasa na kujitolea kwao kwa jamii ilikuwa sehemu kubwa ya maisha yao.

Wakati wa sherehe za kuzaliwa kwake alipokuwa na umri wa miaka 89, Mandela alibuni kikundi cha viongozi wakongwe aliowataka kuendeleza amani duniani.

Dunia inahitaji mtu mpole, mkarimu na wa kujitolea. Bila ya watu kama Mandela kuna uwezekano wa dunia kutumbukia katika migogoro ambayo haitapata wasuluhishi na kwa mtizamo wa wengi ni vigumu kupata mfano wa Mandela duniani.