Shambulio la kujitolea mhanga Benghazi

Benghazi, Libya

Bomu lilotegwa kwenye gari limeuwa watu kama saba kwenye kituo cha ukaguzi cha jeshi karibu na mji wa Benghazi, Libya.

Hilo linafikiriwa ni shambulio la mwanzo la kujitolea mhanga kutokea nchini humo.

Watu kadha walijeruhiwa.

Shambulio hilo limetokea baada ya mkuu mpya wa idara ya usalama mjini Benghazi kupigwa risasi na kuuwawa katika mji jirani wa Derna.

Wapiganaji wamefanya mashambulio kadha mashariki mwa Libya tangu Kanali Gaddafi kuondolewa madarakani mwaka wa 2011.