Papa Francis atetea wanyonge wa vita

Papa Francis akipungia mkono waumini Vatikani

Katika hotuba yake ya mwanzo ya Krismasi, Papa Francis amezungumza mjini Rome juu ya maeneo ya vita duniani.

Alitoa wito kwa pande zote zilizohusika na vita vya Syria ziruhusu msaada kufika kwa wanyonge.

Alisema:

"Maisha mengi yamevunjika katika vita vya Syria na kuchochea chuki na kulipiza kisasi.

Wacha tuendelee kumuomba Mungu awaepushe wapendwa watu wa Syria na maafa zaidi, na kuziwezesha pande zilizohusika na vita kumaliza ghasia na kuruhusu msaada ufike kwa wale wanaouhitaji"

Papa Francis piya alitoa wito kwa mapigano kusitishwa Sudan Kusini na aliwaomba viongozi wa kimataifa kushughulikia zaidi yanayotokea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo alisema mara nyingi haitiwi maanani.

Akizungumza juu ya mamia ya wakimbizi kutoka Eritrea waliozama karibu na kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa mwezi Oktoba, alieleza wasiwasi wake kuhusu wale wanaohatarisha kila kitu ili kutafuta maisha bora.

Piya alizungumzia swala la ukatili majumbani, akitetea wanawake wanaopigwa.