UN kutuma ndege za upelelezi Sudana K.

Image caption Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa nchini Sudan umesema kuwa utatumia ndege za upelelezi kujaribu kuhakikisha idadi ya vijana walioripotiwa kuandamana kwenda kwenye mji wa Bor.

Serikali ya Sudan Kusini ilisema siku ya jumamosi kuwa kulikuwa na maelfu ya vijana ambao ni wafuasi wa kiongozi wa waasi Riek Machar.

Vijana hao waliobeba silaha za jadi na fimbo inaelezwa hawana mafunzo yoyote ya kijeshi, Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC.

Lakini msemaji wa waasi amesema kulikuwa na askari wa kawaida ambao walikuwa wakirejea serikalini. Msimamizi wa mazungumzo kutoka Afrika amewapa Bwana Machar na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir hadi Decemba 31 wawe wameanza mazungumzo.

Karibu watu 1000 wamekufa katika mapigano yaliyochukua mwezi mmoja sasa, huku wengine 121,600 wanahofiwa kuyakimbia makazi yao.

Tayari maelfu ya raia wanatafuta hifadhi ya ukimbizi katika kambi za Umoja wa Mataifa huku wanajeshi zaidi wa kuongeza nguvu wa Umoja wa Mataifa wakiwa wamewasili nchini humo kwa ajili ya kuimarisha usalama wa raia.