Muigizaji wa Fresh Prince afariki

Image caption Avery amefariki kutokana na matatizo ya Moyo

Muigizaji wa Marekani, aliyeigiza katika kipindi maarufu sana cha kuchekesha 'Fresh Prince of Bell Air', James Avery amefariki akiwa na umri wa miaka 68.

Alisifika sana kama Phil Banks kwenye kipindi hicho akishirikiana na Will Smith.

Muigizaji mwenzake Alfonso Ribeiro, alituma ujumbe wa Twitter, akisema amesikitishwa sana na kifo cha James Avery akisema kuwa alikuwa kama babake.

Mkewe Will Smith Jada Pinkett Smith, pia alielezea kusikitishwa kwake kufuatia kifo cha muigizaji huyo.

Avery aliigiza kwenye vipindi vya televisheni ikiwemo Gray's Anatomy na Star Trek: Enterprise.

Pia sauti yake ilisikika katika vipindi kama Teenage Mutant Ninja Turtles na Iron Man.

Lakini anajulikana zaidi kwa uigizaji wake kama jaji na baba katika kipindi cha Fresh Prince of Bel-Air kilichopeperushwa miaka ya tisini.

Avery alifariki kutokana na matatizo ya kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Aidha Avery aliwahi kuwa mwanajeshi kati ya mwaka wa 1968 hadi 969, kabla ya kuanza kujihusisha na vipindi vya tlevisheini.