Data yako iko salama mtandaoni?

Akaunti za watumiaji milioni 4.6 wa mtandao wa kijamii wa Snapchat na namba zao simu zimedukuliwa na watu walioziweka data hizo mitandaoni.

Mtandao wa SnapchatDB ndio ulichapisha data hiyo kwa muda kwenye mtandao ingawa ulificha nambari mbili za mwisho za simu zilizochapishwa.

Hata hivyo data hiyo inasemekana imeondolewa kwenye mtandao.

Udukuzi huu umeripotiwa siku moja baada ya kampuni ya usalama ya Gibson nchini Australia kuonya kuwa watumiaji wa programu hiyo walikuwa katika hatari ya taarifa zao kudukuliwa.

Kampuni ya Gibson hata hivyo ilisema kuwa haikuhusika na udukuzi huo ingawa ilijua kuwa wanaotumia programu hiyo walikuwa natika hatari ya kudukuliwa.

Watu waliofanya udukuzi huo , wamesema kwamba walitumia pengo lililokuwepo na ambalo kampuni ya Gibson ilikuwa kutambua kufanya udukuzi wao.

Programu ya Snapchat imekuwa kwa kasi na hutumiwa na watumiaji wake kutumiana picha ingawa wana uhakika kuwa programu hiyo baadaye hufuta picha hizo.

Programu hiyo pia inawaruhusu watumiaji kutumiana picha na kuweza kupata anwani zao kupitia kwa Facebook