Ni ipi filamu bora zaidi ya 2013?

Image caption 12 years a Slave imegusia swala tete la utumwa

Filamu yenye mada ya kisayansi kwa jina ''Gravity'' pamoja na filamu nyingine kuhusu utumwa nchini Marekani, ''12 Years a Slave'', ni miongoni mwa filamu zinazopigiwa upatu kupata tuzo la filamu bora zaidi katika tamasha la filamu bora zaidi la Uingereza British Academy Film Awards.

Tamasha hili ni sawa la lile la Marekani la Oscars.

''Gravity'' imepata kuteliwa mara 11 katika vitengo mbali mbali, ikiwemo filamu yenye picha bora zaidi na kuwa na muigizaji bora zaidi Sandra Bullock.

"12 Years a Slave'' nayo ilipata kuteuliwa mara kumi ikiwemo kuwa na muigizaji bora zaidi ,Chiwetel Ejiofor muigizaji wa Uingereza mwenye asili ya Nigeria na mtengeza filamu bora zaidi Steve McQueen.

Ejiofor amenukuliwa akisema kuwa anajivunia sana kutokana na dunia kuitambua sana filamu hiyo ambayo ilihusu mateso dhidi ya watumwa wakati wa enzi za utumwa.

Ejiofor alikuwa anaigiza mwafrika aliyetekwa nyara na kuuzwa kama mtumwa katika karne ya kumi na tisa nchini Marekani. Na amesema anajivunia sana pia kwa kuteuliwa kama muigizaji bora katika filamu hiyo katika BAFTA.

Filamu nyingine ya Marekani ambayo mada yake ni uhalifu ''American Hustle'' ilipata kuteuliwa mara kumi huku filamu inayohusu maharamia Somalia, 'Captain Phillips' ikipata uteuzi mara tisa.

Muigizaji mwingine aliyetesa katika filamu ya '12 years a Slave' ni mkenya Lupita Nyong'o ambaye huenda akashinda tuzo la muigizaji msaidizi bora zaidi. Uigizaji wake umewavutia wengi na tangu filamu hiyo kutolewa ameshinda tuzo kadhaa.

Wengine walioteuliwa kushinda tuzo ni Leonardo DiCaprio katika filamu ya ''The Wolf of Wall Street'' na Judi Dench kwa filamu kwa jina ''Philomena.'' Filamu ipi ilitesa 2013?