Kauli yako kuhusu kifo cha Ariel Sharon

Image caption Ariel Sharon zama zake akiwa mwanajeshi

Watu wengi kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakitoa kauli zao kuhusu taarifa za kifo cha Ariel Sharon. Nini kauli yako? tuma ujumbe wako kwenye ukurasa wa facebook bbcswahili

10:10 Beatrice Michael anasema Saharon apumzike kwa amani

10:00 Wengi wamekuwa wakituma ujumbe wa kumlaani sana Ariel Sharon kutokana na matendo yake kwa wapalestina lakini Kassim Yassin kupitia facebook anasema Mola ndiye ajuaye yupi wa motoni na yupi wa peponi,tukumbuke kila mtu ataelekea uko,atauwe gaidi,mchawi,mwizi,kufa wajibu

09:55 John F Minja kupitia kwa ukurasa wa bbcswahili facebook anasema kuwa wakati wa msiba tuyasahau yote aliyowatendea wapalestina na walebanon.Tumsamehe kwa mabaya yote.