Ghasia kwenye kura ya maamuzi Misri

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Jeshi linawataka watu kupiga rasimu ya katiba kura ya ndio

Kulikuwa na ghasia katika siku ya kwanza ya kupigia kura ya maamuzi rasimu ya katiba mpya ambayo huenda ikatoa nafasi ya kuandaliwa kwa uchaguzi mpya nchini humo.

Wafuasi wa Rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi walizua vurugu na hata kusababisha vifo kadhaa.

Katiba mpya itaondolea mbali wamisri katiba aliyoipitisha Morsi na iliyokuwa serikali yake kabla ya jeshi kuwaondoa mamlakani.

Jeshi linataka watu waipigie katiba hiyo kura ya ndio katika shughuli hiyo itakayaoendelea wa siku mbili.

Vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo limetajwa kuwa kundi la kigaidi limesusia kura huyo ya maamuzi.