Mlipuko waua 17 Maiduguri,Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram limekiri kufanya shambulizi hilo

Watu kumi na saba wamefariki mwenye mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mjini Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram, limekiri kufanya shambulizi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa za jeshi mshukiwa mmoja amekamatwa.

Mlipuko huo ulitokea karibu na soko moja mjini humo. Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa waliwaona watu wakitoroka kutoka eneo hilo nguo zao zikiwa na damu.

Kundi la Boko Haram, limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara Kaskazini mwa Nigeria likiishinikiza serikali kukubali sheria za kiisilamu kutumika katika eneo hilo ambako wakazi wake wengi ni waumini wa kiisilamu.

Miili ilionekana ikiwa imetapakaa kote huku shahidi mmoja akiambia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na milipuko mingine midogomidogo