Jua kali lasitisha Australian Open

Haki miliki ya picha
Image caption Viwango vya joto vimefika nyuzi 42

Viwango vya juu vya joto vimewalazimisha waandalizi wa mashindano ya tennis ya Australian Open, kusimamisha mashindano hayo.

Mechi zilizoratibiwa kuchezwa katika viwanja vya nje zimesimamishwa baada ya viwango vya joto kufika nyuzi 42.

Hata hivyo mechi zingine ziliendelea katika viwanja viwili ambavyo vina nyufa na mtambo wa kuthibiti viwango vya joto.

Waandalizi wa mashindano hayo mjini Melbourne walishutumiwa baada ya mchezaji mmoja na kijana mmoja aliyekuwa akisaidia uwanjani kuzirai mapema wiki hii.

Wataalamu wa mabadiliko ya tabia ya nchi nchini humo wameonya kuwa viwango vya joto nchini humo vinaendelea kuongezeka na msimu wa joto umekuwa mrefu na hutokea mara kwa mara.