Makamanda wa jeshi watimuliwa Nigeria

Haki miliki ya picha d
Image caption Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na wapiganaji wa Boko Haram lakini changamoto ni nyingi

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amewafuta kazi makamanda wake wakuu wa jeshi ,na kufanya mabadiliko ambapo amemteuawa mkuu wake wa ulinzi, wakuu wa majeshi ya anga na majini .

Hakuna sababu iliyotolewa kuhusu hatua hiyo .

Mkuu wa mpya wa majeshi Alex Badeh, anatoka kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi la Nigeria limekuwa likihangaika kudhibiti uasi wa kundi la kiislam la , Boko Haram, ambalo limekuwa likiendesha harakati zake zaidi katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi.