Msumbiji: Hatuna washukiwa waliomuua Karegeya

Image caption Kareguya aliuawa nchini Afrika Kusini huku Rwanda ikisema alikuwa adui wake

Polisi nchini Msumbuji wamekanusha madai kuwa wamewakamata watu wanaoshukiwa kumuua mkuu wa zamani wa ujasusi nchini Rwanda Patrick Karegeya.

Msemaji wa polisi nchini humo Joao Machava amesema kuwa hakuna mshukiwa aliyezuiliwa kuhusiana na mauaji hayo ya Patrick Karegeya ingawa kuna raia kadhaa wa Rwanda waliokamatwa nchini humo.

Awali alinukuliwa akisema wanyarwanda kadhaa wamekamatwa na wanatarajiwa kurejeshwa nchini Afrika Kusini.

Marehemu Karegeya alikimbilia uhamishoni nchini Afrika Kusini na alipatikana akiwa amefariki katika hoteli yake mjini Johannesburg January tarehe moja.

Polisi wanaamini kuwa Karegeya aliuawa.