Ribbery na Benzema mahakamani Paris

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Benzema na Ribbery

Wacheza soka wawili mashuhuri duniani, wamefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa kwa kosa la kufanya ngono na kahaba aliyekuwa na umri mdogo.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa hivi, alisema kwamba,Franck Ribery, mchezaji wa Bayern Munich , alimtumia kama zawadi wakati wa sherehe za siku yake ya kuzaliwa mwaka 2009.

Inaarifiwa Ribbery alimpilia msichana huyo tiketi ya ndege aweze kusafiri kutoka Ujerumani Kuja Ufaransa kumtumbuiza Ribbery wakati wa sherehe hizo.

Alisema kuwa pia alilipwa ili afanye ngono na Karim Benzema anayecheza soka yake na klabu ya, Real Madrid.

Kahaba huyo alisema kwamba, aliwaambia wawili, hao kuwa alikuwa mtu mzima wakati huo.

Benzema amekanusha madai ya msichana huyo.

Wachezaji hao wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kila mmoja ikiwa watapatikana na hatia.