Wanajeshi wa Ethiopia wajiunga na Amisom

Haki miliki ya picha
Image caption Wanajeshi wa AMISOM nchini Somalia

Wanajeshi wa Ethiopia hii leo wamejiunga rasmi na wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaoshika doria nchini Somalia (Amisom) ili kutengeza kikosi cha sita cha wanajeshi wa Muungano huo ndani ya Somalia.

Kuna wanajeshi kadhaa wa Ethiopia nchini Somalia,ambao ni sehemu ya wanajeshi wanaopambana na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.

Ethiopia ni nchi pekee ambayo ilikuwa na vikosi vyake nchini Somalia ambao hawakuwa chini ya muungano wa wanajeshi wa AMISOM.

Wanajeshi wa Ethiopia waliingia mara ya kwanza nchini Somalia mwaka 2011 kusaidia iliyokuwa serikali ya mpito, kufurusha wanamgambo wa Al Shabaab kutoka katika miji mikubwa ya Somalia.