Waasi 11 wauawa nchini Mali

Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Ufaransa inaendelea kupunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Mali

Wanajeshi wa Ufaransa wanasema kwamba wamepambana na waasi katika mji wa Tumbuktu Kaskazini mwa Mali ambapo wapiganaji kumi na moja wameuawa.

Msemaji wa jeshi la Ufaransa amesema kuwa wanajeshi mia moja wanaanga na wale wa nchi kavu walihusika katika mapambano hayo.

Aliongeza moja ya kambi za wapiganaji hao iliharibiwa.

Katika oparesheni hiyo mwanajeshi mmoja wa Ufaransa alijeruhiwa.

Mwezi uliopita Ufaransa iliharibu kambi kubwa ya waasi hao katika sehemu hiyo.

Ufaransa inaendelea kupunguza idadi ya wanajeshi wake waliokwenda Mali kupambana na waasi waliokuwa wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo

.