Hakuna aliyesitisha mapigano Sudan-K

Wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini Haki miliki ya picha AFP

Serikali ya Sudan Kusini na wapiganaji wanaendelea kulaumiana kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalianza kutekelezwa Ijumaa.

Msemaji wa waasi, Brigedia Jenerali Lul Ruai, alieleza kuwa wanajeshi wa serikali wameshambulia maeneo yao katika sehemu kadha.

Serikali ilikanusha hayo na iliwalaumu waasi kwa mashambulio.

Kila upande unasema haufikiri kuwa upande wa pili unaweza hasa kudhibiti majeshi yake.

Maelfu ya watu wamekufa katika vita hivyo baina ya jeshi la serikali ya Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa naibu wake wa zamani, Riek Machar.