Mkutano wa Syria wazaa matunda, machache

Ujumbe wa upinzani wa Syria katika mkutano wa Geneva Haki miliki ya picha AFP

Mpatanishi wa Umoja wa Mataifa katika vita vya Syria, Lakhdar Brahimi, anasema kuwa baada ya siku ya pili ya mazungumzo ya amani mjini Geneva, ujumbe wa serikali umesema kuwa

wanawake na watoto wanaweza kutoka maeneo ya kati-kati ya mji wa Homs yaliyozingirwa.

Bwana Brahimi alisema kazi inaendelea kujaribu kufikisha msafara wa misaada hadi mji huo wa Homs - jambo ambalo upinzani umekuwa ukidai.

Alisema kuwa yamefanywa majadiliano kuhusu swala la wafungwa, lakini hawakufikia makubaliano.

Alieleza kuwa asubuhi alifanya mkutano na pande zote mbili katika chumba kimoja, lakini jioni kila ujumbe ulikuwa na chumba chake.

Alisema inavoelekea itifaki hiyo itafuatwa Jumatatu piya.