Ukraine:Upinzani wapata afueni

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shinikizo zamfanya Rais Victor Yanukovych kujumuisha upinzani katika serikali yake

Rais wa Ukraine Victor Yanukovych ameupa upinzani baadhi ya nyadhfa muhimu za serikali katika juhudi za kumaliza maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo kwa majuma kadhaa sasa.

Lakini viongozi hao wa upinzani wamesema kuwa hawako tayari kuchukua nyadhfa hizo huku makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yakiendelea katika mji mkuu wa Kiev.

Kiongozi wa chama cha Ukrain Fatherland Arseniy Yatsenyuk amesema kwamba yeye na viongozi wengine wa upinzani wako tayari kuichukua serikali,lakini akasisitiza kuwa uamuzi huo utafanywa na wapiga kura na wala si rais.

Muhariri wa maswala ya kibiashara katika gazeti la Kiev post Mark Rechkevych amesema kuwa wapinzani hao hawakutaka kuhalilisha mamlaka ya rais huyo.

Upinzani umekuwa ukisisitiza kufanyika kwa uchaguzi wa mapema.

Wakati huohuo waandamanaji wamelizunguka jumba moja mjini Kiev ambapo polisi wa kukabiliana na ghasia wamewekwa.