Waziri wa zamani Malawi akamatwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanaharakati wapinga ufisadi nchini Malawi

Waziri wa zamani wa sheria nchini Malawi, amekamatwa kwa tuhuma za kujipatia fedha chafu.

Tuhuma hizo zinahusishwa na kile kinachosemekana kuwa kashfa ya 'Cashgate' ambapo hadi sasa washukiwa sabini wamekamatwa.

Katika kashfa hii,mamilioni ya dola pesa za serikal ziliibwa kiasi cha kuathiri mishahara ya wafanyakazi wa umma.

Kukamatwa kwa waziri huyo wa zamani, Ralph Kasambara, ni hatua kubwa katika juhudi za kufumbua kashfa hii ambayo inasemekana kuwa ngumu kwa serikali.

Alifutwa kazi kama waziri mwezi Septemba na tangu Novemba mwaka jana amekuwa nje kwa dhamana kwa madai ya kupanga mauaji ya afisaa mmoja wa wizara ya fedha.

Bwana Kasambara pia alitarajiwa kufikishwa mahakamanai Jumanne kumtetea mwanamke aliyehusishwa na kashfa hiyo, hatua ambayo anasema serikali inajaribu kumnyamazisha.

Mashitaka anayokabiliwa nayo ni pamoja na kampuni yake ya sheria kupokea pesa za wizi kutoka kwa serikali

Anakanusha tuhuma hizo akisema kuwa alikuwa waziri wakati huo wala hakuwa mkuu wa kampuni yake.