Michael Schumacher kuanza 'kuamshwa'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Michael Schumacher

Madaktari wanaomtibu mwendeshaji mashuhuri wa magari ya langalanga mjerumani Michael Schumacher, wameanza kupunguza dawa waliyompa ya kumfanya kuwa katika hali ya mahututi ili kujaribu kumrejeshea fahamu tena.

Bingwa huyo mara saba wa mbio za langalanga aliteleza na kuanguka huku akigonga kichwa chake kwenye jabali katika milima ya Alps alipokuwa akiteleza kwenye barafu.

Maneja wa Schumacher (Sabine Kehm) amesema kuwa hatua ya kumfanya atembee tena itachukua muda mrefu.

Wataalamu wa matibabu wanasema ni vigumu kukadiria hali itakavyokuwa iwapo hatua hiyo ya kumuamsha itafaulu.

Madaktari walimpa Michael Schumacher dawa ya kumfanya kupoteza fahamu kabisa Michael Schumacher baada ya ajali hiyo ili kupunguza mikwaruzo aliyopata pembezoni mwa ubongo wake.

Amefanyiwa operesheni mbili ili kuondoa mgando wa damu.