Hofu baada ya mashambulizi Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na Boko Haram wanaowashambulia watu kiholela

Maafisa wa utawala nchini Nigeria wanasema kuwa zaidi ya watu elfu mbili wametoroka makwao baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kiisilamu kushambulia kijji kimoja Kaskazini mwa nchi.

Watu hamsini na wawili waliuawa katika kijiji cha Kawuri kilicho katika jimbo la Borno siku ya Jumapili.

Shambulizi hilo limesemekana kusababishwa na kundi la wanamgambo la Boko Haram.

Zaidi ya watu 30 pia waliuawa siku hiyo hiyo wakatio ambapo kanisa liliposhambuliwa katika jimbo jirani la Adamawa.