UN kulinda wanyamapori DRC

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Baadhi ya wanyamapori wanaouawa kufadhili makundi ya wapiganaji DRC

Makundi ya kuhifadhi wanyama pori yamepongeza hatua zilizochukuliwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa kukabiliana na makundi ya watu waliojihami ambao hufadhili oparesheni zao kupitia kwa ulanguzi wa wanyama pori.

Azimio jipya la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kuwapiga marufuku ya kusafiri washukiwa wa ulanguzi wa wanyamapori pamoja na kupiga tanji mali za wanaohusika na biashara hiyo haramu ya wanyama pamoja na bidhaa za wanyama pori katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Biashara hii haramu inasemekana kuendelezwa kwa lengo la kuunga mkono makundi ya waasi yanayoendesha vita nchini humo.

Umoja wa mataifa umekuwa ukionya kwamba uwindaji wa pembe za Ndovu umekuwa ukitumiwa kufadhili makundi ya wapiganaji na hivyo basi kusababisha kupungua kwa idadi ya Ndovu.

Azimio sawa na hilo lilipitishwa mapema wiki hii kutokana na hali ilivyo katika Jamhuri ya Afrika ya kati.