Sudan yasimamisha shughuli za misaada

Matabibu wa ICRC Haki miliki ya picha Reuters

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, limeombwa lisimamishe shughuli zake nchini Sudan.

Mwaka jana shirika hilo lilisaidia watu zaidi ya milioni moja na nusu walioathiriwa na vita.

ICRC inasema imepata barua kutoka kwa wakuu wa Sudan kusema kuwa mwaka huu kuna matatizo ya kiufundi kuhusu mipango ya misaada.

Shirika hilo linatoa misaada ya chakula, maji, huduma za afya, zana za kilimo na misaada mengine, hasa katika jimbo la Darfur.

Sudan imesimamisha kwa muda au kuyafukuza mashirika kadha ya misaada yenye shughuli nchini humo.