Polisi wavamia msikiti Mombasa

  • 3 Februari 2014
Ramani

Watu 3 akiwemo polisi wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa kwenye ghasia katika mji wa Mombasa, Kenya, baada ya polisi kuvamia msikiti unaosemekana kutoa mafunzi ya itikadi kali za dini ya kiisilamu

Polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na risasi za raba dhidi ya waandamanaji na kuwakamata watu 100.

Viongozi wa mombasa wamelaani kitendo cha polisi wakisema kuwa ni kinyume na sheria.

Mashekhe wawili ambao wakihubiri katika msikiti wa Masjid Mussa walipigwa risasi na kuuliwa na watu wasiojulikana katika miezi ya karibuni.

Polisi wa Kenya wameuhusisha msikiti huo na kuajiri wapiganaji wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al Shabaab, ambalo mwaka jana lilishambulia jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi.