Upinzani wasambaratika Afrika Kusini

Image caption Daktari Mamphela Ramphele

Mpango wa kukiunganisha chama rasmi cha upinzani Democratic Alliance na chama kimoja kidogo cha Agang kwa lengo la kukabiliana na chama tawala cha ANC katika uchaguzi mkuu ujao nchini Afrika Kusini umegonga mwamba.

Wakati mpango huo ulipotangazwa juma lililopita ,kiongozi wa chama hicho kidogo cha Agang ,Daktari Mamphela Ramphele alipewa wajibu wa kuwania urais.

Lakini akitangaza kuwa mpango huo umetibuka,chama cha Democratic Alliance kimeshtumu bwana Ramphele kwa kukiuka makubaliano yao ya kusimamia urais.

Umesema kuwa raia wengi wa Afrika Kusini watashangazwa na ushirikiano huo uliotarajiwa kuwa wa kihistoria.

Daktari Ramphele ambaye ni mwanaharakati na msomi alikuwa mshiriki mkuu wa mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Steve Biko ambaye aliteswa na kufariki korokoroni mnamo mwaka 1977.