Polisi watawanya wachimba migodi A.Kusini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachimba migodi wamekuwa wakiandamana kutaka nyongeza ya mishahara

Polisi nchini Afrika Kusini wametumia maguruneti na risasi za mipira kuwatawanya zaidi ya wachimba migodi ambao walikuwa wanaandamana karibu na mji wa Rustenburg.

Polisi wanasema kuwa wachimba migodi hao katika mojawpao ya migodi ya kampuni ya Anglo-American,walikuwa wanabeba silha hatari na kutishia kuwaondoa wafnyakazi wenzao kutoka mgodini.

Polisi wamewakamata watu wawili.

Takriban wanachama elfu nane wa muungano wa wachimba migodi na wajenzi walifanya mgomo mnamo mwezi january wakitaka kuongezwa mshahara.

Mgomo huo ni mkubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini Afrika ya kusini katika sekta ya uchimbaji wa madini ya platinum tangia mgomo wa mgodi wa marikana mnamo mwaka 2012 ambapo maafisa wa polisi waliwapiga risasi na kuwauawa wachimba mgodi 34.