Viongozi wa maandamano Ukraine waonywa

Serikali ya Russia imewatahadharisha viongozi wa muungano wa upinzani na waandamanji wanaodhibiti maeneo ya bustani za Kiev Ukraine wakome kuchochea uhamsama baina ya umma na Serikali ya Rais Viktor Yanukovych .

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waandamanaji Kiev

Afisi ya wizara ya maswala ya nje ya Russia imewataka viongozi hao wa upinzani kuendelea mbele na jitihada za kutafuta suluhu ya mgogoro ambao unatishia ustawi wa Ukraini .

KUIOKOA UKRAINE

Maelfu ya waandamanji wamekita kambi katika Bustani za mji wa Kiev mbali na kutwaa majengo ya serikali tangu Rais Viktor Yanukovych kutupilia mbali makubaliano ya kiuchumi na Umoja wa Ulaya na badala yake Kupokea dola bilioni Kumi na tano kutoka Russia .

Serikali ya Marekani na Muungano wa mataifa ya Bara Ulaya zinaonekana zinajiandaa kuipa Ukraine msaada mkubwa ilikuisaidia kutekeleza majukumu yake kiuchumi mbali na kulipa madeni yake.

Rais wa Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso amesema kuwa Umoja wa Ulaya hautashindania usemi katika siasa na uchumi wa Ukrane dhidi ya Russia.

DENI KUBWA

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Polisi nchini Ukraine

Viongozi wa umoja wa Ulaya pamoja na Serikali ya Marekani wameahidi kutoa mabilioni ya fedha kuinusuru serikali ya Rais Viktor Yanukovych iwapo tu atakubali mabadiliko ya kimsingi ya mfumo wa serikali yake ili kuwajumuisha viongozi wa makundi ya Upinzani kuunda serikali ya mseto .

Mapendekezo mengine ni kupunguzwa kwa mamlaka ya Rais la sivyo angatuke mamlakani.

Hata hivyo haijabainika kufikia sasa iwapo waandamanaji watakubali mkataba kama huo ama wataendelea na maandamano hayo ya uasi mjini Kiev.