Misri: Al-Sisi hana uchu wa madaraka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Field Marshall Al-Sisi

Jeshi la Misri limekanusha ripoti za gazeti moja nchini Kuwait kuwa mkuu wa majeshi nchini Misri,Field Marshall, Abdel Fattah al-Sisi, atagombea urais.

Gazeti la al-Seeyassah, limemnukuu Field Marshall akisema kuwa hana budi ila kukubali wito wa wananchi wa Misri.

Lakini katika taarifa rasmi kupitia kwa mtandao wa kijamii, msemaji wake amesema kuwa ripoti hizo sio sawa na kuwa tangazo lolote la Al-Sisi kuwania urais atalitoa mbele ya wananchi wa Misri.

Field Marshall al-Sisi anaaminika kuwa nguvu au shinikizo la hatua ya jeshi la Misri kumuondoa mamlakani aliyekuwa Rais Mohammed Morsi.