Sisi huenda atawania Urais

Haki miliki ya picha AP
Image caption Field Marshal Abdel Sisi

Gazeti moja nchini Kuwait limedai kwamba mkuu wa majeshi nchini Misri, Field Marshal Abdel Fattah al Sisi, amesema kuwa atagombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao.

Gazeti la Al Seeyassah limemnukuu bwana Sisi akisema kuwa hana budi ila kusalimu amri na kukubali matakwa ya wamisri kwa kugombea kiti hicho.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wafuasi wa Sisi

Sisi alikuwa anatarajiwa kuwania kiti cha Urais licha ya jeshi kukataa kudhibitisha niya hiyo.

Sisi alipata umaarufu mkubwa sana baada ya kuongoza mapinduzi ambayo ilimngoa mamlakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi.

Wakosoaji wanahofu kwamba kuchaguliwa kwa bwana Sisi huenda kukairejesha Misri katika enzi za utawala wa kiimla, miaka mitatu baada ya vuguvugu lililomwondoa madarakani Hosni Mubarak.