Milipuko miwili yaitikisa Cairo

Image caption Ramani ya Misri

Mabomu mawili yamelipuka karibu na mji mkuu wa Misri, Cairo katika daraja linalopita juu ya kizuizi cha polisi.

Msemaji wa polisi Jenerali Mahmoud Farouk, yalilenga magari mawili ya polisi wa kupambana na ghasia yaliyokuwa yameegeshwa katika mji wa Giza kushika doria katika msikiti uliopo karibu kabla ya swala ya Ijumaa.

Zaidi ya polisi watatu wamejeruhiwa. Polisi wamezingira eneo hilo. Kumekuwa na maandamano ya mara kwa mara kila Ijumaa nchini Misri tangu jeshi limwondoa madarakani rais aliyezingatia itikadi za kiislamu Mohhamed Morsi mwezi Julai mwaka uliopita.