Waziri wa uhamiaji wa Uingereza ajiuzulu

Mark Harper

Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Mark Harper, amejiuzulu baada ya kujulikana kuwa amemuajiri mtu asiyekuwa na kibali cha kubaki nchini.

Alieleza kuwa alidanganywa na mwanamke mmoja aliyemuonesha nyaraka za bandia, alipomuajiri kusafisha nyumba yake.

Bwana Harper alisema kwa sababu alichangia kupitisha bungeni sheria ngumu kuhusu uhamiaji, alihisi inambidi kuwajibika zaidi kushinda wengine.

Chama cha Conservative kimeahidi kupunguza idadi ya watu wanaohamia Uingereza kutoka malaki na kuwa elfu kadha tu.