Bintimfalme Hispania ahojiwa mahakamani

Image caption Bintimfalme Cristina wa Hispania

Binti Mfalme wa Hispania Bi Cristina amefika mahakamani ili kuhojiwa kuhusiana na kashfa ya ufisadi ikimhusisha na biashara za mume wake.

Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa mtu kutoka familia ya kifalme nchini Hispania kufikishwa mahakamani akikabiliwa na uchunguzi wa makosa ya udanganyifu.

Mume wake Inaki Urdangarin anatuhumiwa kuiba mamilioni ya fedha za umma kutoka serikali za mikoa.

Binti Mfalme na mumewe wamekana kuhusika na makosa hayo na hawajafunguliwa mashitaka.