Mchimba migodi auwawa Afrika Kusini

Wachimba migodi wa Anglo American Platinum  mwaka 2012 Haki miliki ya picha Reuters

Wakuu wa Afrika Kusini wanachunguza kifo cha afisa wa chama cha wafanyakazi kwenye mapambano na polisi wakati wa mgomo katika mgodi wa dhahabu nyeupe.

Msemaji wa polisi alieleza kuwa mtu huyo alipigwa risasi na kuuwawa Ijumaa, wakati polisi walipojaribu kuwatawanya waandamanaji katika barabara inayoelekea kwenye mgodi katika jimbo la Limpopo, kaskazini mwa nchi.

Lakini alisema hakuna hakika ikiwa mtu huyo alipigwa risasi na polisi au walinzi waliokuwako hapo.

Kampuni inayomiliki mgodi huo, Anglo-American Platinum, imesema mtu aliyeuwawa ni afisa wa chama cha wafanyakazi cha AMCU.