Mwanamfalme mahakamani Uhispania

Image caption Mwanamfalme Cristina

Mwana wa kike wa mfalme wa Uhispania anatarajiwa kufika mahakamani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha masaa machache yajayo ili kujibu mashitaka ya udanganyifu.

Mwana mfalme Cristina ,mtoto wa mwisho wa kike wa mfalme Juan Carlos anatarajiwa kuhojiwa na jaji mmoja mjini Mallorca.

Ni mara ya kwanza katika historia ya Uhispania kwa mtu wa familia ya kifalme kufikishwa mahakamani.

Anachunguzwa kuhusiana na biashara ya mumewe ambaye anatuhumiwa kuiba mamiloni ya madola ya fedha za umma.

Mumewe Inaki Urdangarin, anadaiwa kupora mamilioni ya dola pesa za umma kupitia kwa serikali za majimbo.

Ijapokuwa wawili hao hawajashtakiwa wamekana madai hayo.

Kesi hiyo ya mda mrefu imeiharibia sifa familia ya mfalme huyo mbali na kuondosha imani ya raia kuhusu ufalme.