Misaada ya chakula yaelekea mjini Homs.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption makaazi yaliobakia kuwa mahame mjini Homs Syria

Umoja wa mataifa unataraji kuwafikishia chakula na dawa raia waliokwama katika mji wa Homs kufuatia vita vikali kati ya waasi na vikosi vya serikali.

Msafara wa misaada hiyo unatarajiwa kuingia katika mji huo ikiwa ni siku ya pili ya makubaliano ya muda ya kusitisha vita kati ya serikali na waasi.

Siku ya ijumaa zaidi ya watu 80 waliondolewa katika maeneo ya waasi ambayo yamezingirwa kwa takriban mwaka mmoja na nusu sasa.

Wengi wa wanaoondoshwa katika eneo hilo wameonekana wachovu.

Baadhi yao wamesema kuwa hawajala mkate kwa takriban miezi mitano sasa.