Waislamu wote wataihama CAR

Ghasia za Jamhuri ya Afrika ya Kati Haki miliki ya picha AP

Afisa mwandamizi wa shirika la kutetea haki za kibinaadamu ameiambia BBC kwamba baada ya siku au majuma machache Waislamu wote wataihama Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mkurugenzi wa maafa wa Shirika la Kutetea haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, Peter Bouckaert, amesema matokeo hayo yatakuwa mabaya kwa uchumi wa nchi kwa sababu Waislamu wanadhibiti soko la nyama na biashara kadha.

Bwana Bouckaert amesema watu tisa wameuwawa katika mji mkuu, Bangui, na Jumapili aliona Muislamu akipigwa mapanga hadi kufa.