Mamia wahamishwa maeneo ya Vita-Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafanyajazi wa kutoa misaada ya kibinadam mjini Homs

Wafanyakazi wa huduma za misaada nchini Syria wamewahamisha raia wengi wao wakiwa watoto, wanawake na wazee kutoka mji wa kati wa Homs.

Mashambulizi ya risasi na makombora yanaendelea kupigwa mjini humo huku raia wakiukimbia mji huo.

Zaidi ya raia 600, wengi watoto na wanawake, wamehamishwa kutoka mji wa Homs katikati mwa Syria huku mashambulizi yakifanyika mara kwa mara licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali na waasi.

Katika kipindi fulani wafanyikazi wa kutoa misaada walikwama walipojipata wamenaswa kwenye eneo hilo la mashambulizi yaliosababisha vya watu kadhaa.

Shirika la Umoja wa Mataifa na lile la kutoa misaada la Kimataifa la Msalaba mwekundu ICRC, walifanikiwa kufikisha misaada kidogo tu kwa wale ambao huenda bado hajamudu kutoka eneo hilo ambalo limekuwa wanajeshi wa serikali wamekuwa wakifanya mashambulio hilo kutwaa uthibiti wake kutoka kwa wanajeshi wa waasi.

Waliokolewa walionekana kudhoofika sana kutokana na ukosefu wa chakula na huduma nyenginezo muhimu huku wakikumbwa na taaharuki kubwa wakihofia maisha yao.

Wamekuwa wakiishi katika eneo hilo ambalo limekumbwa na mashambulizi ya kila siku kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Mazungumzo ya kusitisha mapigano yaliyofanyika huko Geneva, yaliidhinisha azimio la kusitisha mapigano hadi hiyo jana lakini gavana wa Homs ameomba muda uongezwe kwa angalau siku tatu ili kuwe na mwanya kwa raia wapatao 900 kuondoka kutoka eneo hilo.

Wengi wa raia wa Syria wameonyesha kutokuwa na amani na mazungumzo hayo yanayoendelea mjini Geneva, wakiyataja kama unafiki wakisema suluhu la Syria litatoka nchini Syria na kutoka kwa raia wa nchi hiyo wenyewe.

Mjini Allepo nako, wanaharakati wanasema watu 11, wameuawa kutokana na mashambulizi ya mabomu yaliodondosha na ndege za serikali ya Syiria.

Vita vya Syria vimesababisha vifo vya Maelfu ya watu na maeneo mengi kuharibiwa kabisa.