NRM kinamtaka Museveni kugombea 2016

Image caption Rais Yoweri Museveni

Wabunge wa chama tawala cha NRM wamempendekeza Rais Yoweri Museveni kuwa mgombea wao wa urais, katika uchaguzi mkuu wa Uganda wa mwaka 2016.

Pendeklezo hilo lilitolewa katika kikao cha faragha cha NRM, kinachoendelea katika chuo cha uongozi Kyankwanzi.

Pendekezo hilo lilitolewa na Mbunge wa vijana wa chama hicho, Evelyn Anite aliungwa mkono na wabunge wote wa chama hicho bila pingamizi.

Wabunge hao walisema kuwa pendekezo lao limetokana na Rais Museveni kufanikisha uthabiiti, usalama na demokrasia nchini Uganda katika kipindi alichotawala huku wakimsihi kuwania urais mwaka 2016.

Wameahidi kumuunga mkono.

Hata hivyo Museveni hakutoa tamko lolote kuhusu pendekezo la wabunge hao. Kumekuwa na tetesi nchini Uganda kuwa Museveni anamuandaa mwanawe Brigedia Muhoozi Kainerugaba kumrithi.