Mwanawe Rais Zuma matatani

Image caption Gari aina ya Porsche likiendeshwa vibaya

Sheria ni msumeno hukata pande zote.

Mwanawe Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Duduzane Zuma huenda akashitakiwa kwa makosa ya kuendesha vibaya gari na kumuua mwanamke mmoja huku akiwajeruhiwa watu kadhaa.

Hata hivyo maafisa wa Polisi ambao wanafanya uchunguzi bado wamekata kutoa maelezo zaidi kuhusiana na ajali hio iliyohusisha gari lake la kifahari na basi la usafiri wa umma tarehe moja mwezi Februari na kumuua mwanamke mmoja.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa Duduzane Zuma, alikuwa anaendesha gari aina ya Porsche wakati ajali ilipotokea katika mtaa wa kifahari wa Sandton mjini Johannesburg.

Dududzane ambaye ni mafnyabishara huenda akashitakiwa

Mtu mmoja alifariki na wengine wawili kujeruhiwa.

Kesi hii bila shaka inaibua hisia za kisiasa kwa upande wa Rais Zuma ambaye serikali yake imekuwa ikikabiliwa na tuhuma za uifisadi pamoja na kukarabati nyumba yake kwa mamilioni ya dola pesa za umma.

Mnamo siku ya Ijumaa , Rais Zuma alitangaza kuwa uchaguzi utafanyika tarehe 7 mwezi Mei katika kile alichosema ni fursa ya kujenga upya demokrasia ya Afrika Kusin, miaka 20 tangu kumalizika kwa enzi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Upinzani umedai kuwa polisi walimshughulikia Dududzane visivyo na hata kukosa kumpima ikiwa alikuwa amelewa kupindukia. Walimsaidia kuondoa gari lake kutoka eneo la ajali badala ya kulipeleka kituoni kama ushahidi.