Huduma kwa majeruhi Burundi

Image caption Athari za mafuriko Burundi

Siku mbili baada ya kutokea mafaa kutokana na mvua iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya sitini nchini Burundi, majeruhi zaidi ya mia moja hamsini wanapokea huduma katika hospitali mbalimbali mjini Bujumbura.

Baadhi yao wako nje katika mahema. Lakini waathirika wengine ambao wamepoteza makaazi yao wamepiga kambi kwenye mashule na makanisa mbalimbali.

Waathirika hao wanalalamika kwamba hawajapata msaada wowote na hususan chakula licha ya serikali kutangaza kwamba itawapatishia huduma za kimsingi za dharura aidha chakula na mahema .

Na hayo ni wakati ambapo serikali ya Burundi imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa haraka iwezekanavyo misaada kwa waathiriwa.

Takwimu za muda zinataja kwamba watu elfu kumi na mbili ndiyo wameathirika