Wajumbe wa Korea Kusini na Kaskazini wakutana

Haki miliki ya picha
Image caption Wajumbe wa Korea Kusini na Kaskazini

Maafisa kutoka Korea Kaskazini na Korea Kusini wamefanya mkutano wa kwanza wa ufunguzi katika kijiji kimoja mpakani mwa mataifa hayo mawili.

Ni mkutano mkubwa kati ya utawala wa Pyongang na Seoul kuwahi kufanyika katika kipindi cha miaka sita iliyopita, huku kila upande ikiwakilishwa na watu mashuhuri.

Hakuna ajenda maalum kuhusu mazungumzo hayo, lakini mwaandishi wa BBC anasema Korea Kusini, inatafuta hakikisho kuwa misururu ya mikutano ya kuungana yatafanyika hatimaye mwezi huu.

Korea Kaskazini nayo inataka kuthibitishia mshirika wake mkuu, China, kwamba sasa mazingara ni imara kwa China kumualika kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Mkutano huo umeandaliwa baada ya Korea Kaskazini kuomba ufanyike.