Waathirika Homs kupata msaada

Haki miliki ya picha .
Image caption Mji wa Homs nchini Syria ambao umeathiriwa na mapigano

Mashirika ya misaada nchini Syria yana matumaini ya kuwapelekea msaada wa chakula na dawa hii leo watu walio mjini Homs. Kuna matumaini kuwa zoezi la kuwaondoa Watu waliokwama katika mji huo litafanyika.

Mamia ya Wanawake, watoto na wazee waliondolewa mjini humo wakati ambao pande mbili zinazohasimiana zilipokubaliana kusimamisha mapigano.

Mazungumzo kati ya Serikali na upinzani yanaendelea siku ya jumanne wakati ambapo wapatanishi wa kimataifa wakijaribu kuangalia namna ya kupeleka misaada kwa watu walioathiriwa na mapigano katika miji mbalimbali nchini Syria.

Mazungumzo kati ya pande mbili pia yatahusisha kupata namna ya kukomesha machafuko na mipango ya uundwaji wa Serikali ya mpito.