Utovu wa usalama wakithiri S.Kusini

Image caption Maelfu wanakabiliwa na tisho la usalama mjini Leer

Maelfu ya watu nchini Sudan Kusini wanaoishi msituni karibu na mji wa Leer wanakabiliwa na mazingia hatari ya kiusalama.

Hii ni kwa mujibu wa shirika la misaada ya MSF ambalo wafanyakazi wake walilazimika kutoroka vita wiki mbili zilizopita.

Walilazimika kwenda na wagonjwa waliokuwa mahututi, lakini sasa wamepungukiwa na dawa huku hali ya usalama ikiendelea kuzorota.

Pande zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini, zilitia saini mkataba wa kusitisha vita mwezi jana lakini mapambano yangali yanaendelea.

Waasi wanatuhumu majeshi kwa kushambulia mji wa Leer ambao ni makao kwa kiongozi wa waasi, Riek Machar

Shirika la MSF halina tena uwezo wa kuwasiliana na nusu ya wafanyakazi wake 240 katika hospitali ya Leer.