Sudan Kusini yatetea majeshi ya UG

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Mkutano wa amani kati ya waasi na serikali umeanza mjini Addis Ababa Ethiopia

Waziri wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin, ametetea kuwepo kwa wanajeshi wa Uganda Nchini Mwake.

Marekani na Ethiopia zimetaka kuondolewa mara moja kwa wanajeshi hao, hiyo ikiwa mojawepo ya masharti toka kwa waasi waliomo kwenye mazungumzo ya amani huko Addis Ababa, Ethiopia.

Lakini bwana Benjamin anasema Sudan Kusini inafaa kukubaliwa kuwa na mshirika na kwamba wanajeshi wa Uganda watasalia Nchini mwake.

Hata hivyo ameahidi kuwa hawataruhusiwa kuendesha shughuli zao karibu na mpaka wa mataifa hayo mawili ili kuzuia mzozo wa kikanda.

Aidha Bwana Benjamini anasema kuwa huenda uchaguzi mkuu Nchini Sudan Kusini utafanyika mwaka ujao kama ulivyopangwa.