6 wauawa kwenye mlipuko Mogadishu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomu lilikuwa limetegwa ndani ya gari

Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka katika lango kuu la kuingilia uwanja mkuu wa ndege mjini Mogadishu Somalia.

Watu 6 wameripotiwa kuuawa huku wengine 10 wakijeruhiwa.

Duru zinasema kuwa mlipuko huo ulitokea karibu na eneo la kuegesha magari. Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu anasema kuwa gari lililokuwa na bomu hilo liligonga gari la Umoja wa Mataifa lenye uwezo wa kuhimili risasi kabla ya bomu kulipuka.

Moshi mkubwa umeripotiwa kufuka kutoka katika eneo hilo.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa raia wa kawaida pamoja na walinzi wa maafisa wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa waliojeruhiwa

Uwanja huo wa ndege wa kimataifa ni makao kwa majeshi wa Muungano wa Afrika AMISOM, balozi na ofisi za Umoja wa Mataifa. Wanamgambo wa Al Shabaab wamekiri kutekeleza shambulizi hilo.