Mchezaji wa kwanza wa Togo, Sochi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mchezo wa Skiing

Macho yote yataelekezwa mjini Sochi, Urusi leo hii wakati ambapo Togo itawakilishwa katika michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi kwa mara ya kwanza.

Mathilde Amivi Petitjean mwenye umri wa miaka 19 anashiriki katika mbio za Cross country za kilomita 10.

Mzaliwa wa Afrika Magharibi, Mathilde Amivi Petitjean alihamia Ufaransa na kuishi katika eneo la Rhones-Alps kama mtoto akiwa na umri wa miaka miwili na kujifunza mchezo wa kuteleza kwa barafu.

Mashindano atakayoshiriki, ni moja ya michezo inayochosha sana katika mashindano hayo ya olimpiki.

Wachezaji wanaanza baada ya sekunde thelathini ya kila mchezaji na kuwaruhusu wanaokwenda mwendo wa polepole kuondoka kwanza huku wenye kasi kubwa zaidi wakiweza kuwashinda katika mkondo huo wa kilomita 10.

Licha ya nafasi atakayomaliza, atakuwa ameweka historia ya kuwa raia wa kwanza wa Togo kushiriki michezo ya Olimpiki ya msimu baridi.