Syria:Hali yatokota amani ikisubiriwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zaidi ya watu 200 wamekuwa wakiuawa kila wiki nchini Syria

Wajumbe wa Marekani na Urusi wanatarajiwa kujiunga na mazungumzo ya amani yanayolenga kusitisha vita kati ya serikali na wapiganaji wa upinzani mjini Geneva.

Bado pande zinazozozana hazijapiga hatua zozote kwa siku za kwanza tatu ambapo mazungumzo hayo yalifanywa.

Wakereketwa Nchini Syria wanasema kuwa kumekuwa na mapigano maeneo mengi ya nchi hiyo.

Aidha shirika la kutetea haki za kibinadamu, limesema kuwa takriban watu 200 wamekuwa wakiuawa kila siku kwa majuma matatu yaliyopita huku kila upande unaozozana, wapiganaji na serikali zikitaka kuthibiti mji huo.

Mapigano makali yameshuhudiwa mpakani mwa Lebanon ambapo majeshi ya Syria na washirika wao Hezbollah wakijaribu kila wawezalo kuudhibiti mji wa Yabroud.

Ndege za serikali zimeonekana zikishambulia maeneo hayo kwa makombora.

Jitihada za kujaribu kufikisha misaada ya kibinadamu Nchini Syria bado zinaendelea lakini Urusi inasema mkutano wa leo unachukuliwa kama wa dharura ili kuokoa hali katika taifa hilo.