Kimbunga kupiga tena nchini Uingereza

Haki miliki ya picha PA
Image caption Makazi ya watu yakiwa yamezingirwa na maji

Kimbunga kinatarajiwa kupiga tena nchini Uingereza.wahandisi wamekuwa katika hati hati usiku mzima kurejesha umeme kwenye majengo zaidi ya 25,000 yaliyokatika umeme kutokana na kimbunga na upepo mkali vilivyojitokeza siku ya jumatano.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imetoa taadhari ya kutokea mvua, upepo na barafu, huku ikitoa matangazo ya taadhari 17 katika baadhi ya maeneo ya Gloucestershire, Berkshire, Surrey na Somerset, na kutabiri kutokea kwa madhara.

Makazi ya watu katika maeneo ya Wales,West Midlands,Cheshire, kaskazini mwa Shropshire na kusini magharibi mwa Uingereza yalikosa nishati ya umeme baada ya kimbunga cha siku ya jumatano.

Taasisi ya mazingira nchini humo imetoa matangazo ya taadhari zaidi 350 hasa katika maeneno ya kusini mwa Uingereza na Midlands.